Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amezindua rasmi mpango wa usambazaji wa majiko banifu wilayani humo, akisisitiza umuhimu wa matumizi yake katika kulinda mazingira na kupunguza ukataji ovyo wa miti.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Machi 28, 2026, amesema majiko hayo yatasaidia kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, hivyo kuchangia juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira. Aidha, amepongeza utekelezaji wa mpango huo na kuomba uongezwe ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Katika mpango huo, serikali imetoa ruzuku ya asilimia 75 ya gharama za majiko hayo, ambapo mwananchi atachangia asilimia 25 pekee, sawa na shilingi 12,200 badala ya shilingi 80,000.
Akizungumzia ubora wa majiko hayo, Mkurugenzi wa kampuni ya Greenway Ecomama kutoka mkoani Iringa Sabitina Makweta, iliyopata zabuni kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), amesema majiko hayo yanatumia kiasi kidogo cha mkaa na kuni, hivyo kusaidia kuhifadhi mazingira.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Abednego Madole, amesema wilaya hiyo imepokea majiko 1,309 ambayo yatagawiwa katika maeneo mbalimbali katika awamu ya sasa.
Baadhi ya wananchi waliopata majiko hayo wameishukuru serikali kupitia REA kwa kuwapatia fursa hiyo, wakisema hatua hiyo itawasaidia hasa wanawake kupunguza muda wanaotumia kupika. Pia wameomba mpango huo uendelezwe katika awamu nyingine ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi
Mkurugenzi wa kampuni ya Greenway Ecomama kutoka mkoani Iringa Sabitina Makweta akielezea majiko hayo banifu jinsi yanavyofanya kazi wakati wa uzinduzi kwa wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Machi 28, 2026 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi
Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Abednego Madole, wa uzinduzi wa majiko banifu wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Machi 28, 2026 huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndie mgeni rasmi
Post a Comment