RAIS SAMIA AMTEMBELEA HOSPITALI BABA MZAZI WA MWENYEKITI WA ACT-WAZALENDO NA KUMJULIA HALI PACOME WA YANGA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemtembelea na kumjulia hali Sheikh Rashid Hamad Othman, ambaye ni Baba Mlezi wa Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, alikolazwa akipatiwa matibabu.


Rais Samia akimjulia Hali baba wa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Mhe. Samia pia amemjulia hali kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.


Pacome alipata majeraha ya mguu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Yanga ilipocheza dhidi ya JKT Tanzania, Juni 30, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan akimjulia Hali mchezaji wa Yanga Pacome

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم