Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye kikao chake cha kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Unyanyembe Kata ya Uchunga wilayani humo Jalai 14, 2026
Na Sumai Salum-Kishapu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Josephat Limbe, amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kijiji cha Unyanyembe, Kata ya Uchunga, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Halmashauri wa kuwafikia wananchi, kusikiliza kero zao na kutafuta suluhisho kwa wakati.
Katika ziara hiyo, Mhe. Limbe amesaidia kupatikana kwa mifuko zaidi ya 140 ya saruji pamoja na fedha zaidi ya Sh. 500,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi na ukarabati wa majengo ya Zahanati ya Unyanyembe, baada ya wananchi kueleza changamoto ya upungufu wa miundombinu katika kituo hicho.
Wananchi wamebainisha kuwa zahanati hiyo inahitaji majengo ya ziada, hususan jengo la huduma za mama na mtoto, pamoja na ukarabati wa baadhi ya majengo yaliyopo. Akizungumza baada ya kusikiliza changamoto hiyo, Mhe. Limbe ameahidi kutoa mchango wake binafsi kusaidia kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo.
Aidha, amesema atafanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Emmanuel Johnson ili kupitia vyanzo vya mapato ya ndani kutenga fedha zitakazosaidia ujenzi wa boma la zahanati hiyo.
“Ushirikiano kati ya Serikali na wananchi ni msingi muhimu katika kuharakisha maendeleo. Tukiunganisha nguvu zetu, tutaweza kuboresha huduma za kijamii na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,” amesema Mhe. Limbe.
Katika hatua nyingine, ametembelea zahanati hiyo ya Kijiji Cha Unyanyembe amemuelekeza Mtendaji wa Kata ya Uchunga kuhakikisha anafuatilia kwa haraka upatikanaji wa ramani ya zahanati hiyo na kuhamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wake ili kuwezesha Serikali kutenga bajeti ya kukamilisha mradi huo muhimu.
Diwani wa Kata ya Uchunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Lukas Manyegule akizungumza kwenye kikao cha Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu cha kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kijiji cha Unyanyembe Kata ya Uchunga wilayani humo Jalai 14, 2026
Katika mkutano huo wa kusikiliza wananchi, wakazi wa Unyanyembe wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, zikiwemo upungufu wa miundombinu katika Zahanati ya Unyanyembe, ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari, ukarabati wa Shule ya Msingi Unyanyembe, upanuzi wa huduma ya umeme katika baadhi ya vitongoji, ubovu wa barabara ya Ngundangali–Kakola kupitia Nida, ukosefu wa mtandao wa simu katika baadhi ya maeneo pamoja na hitaji la kusambazwa kwa huduma ya maji katika vitongoji vya Kasenya, Ugalama,Mwamakelemo navinginevyo.
Akijibu changamoto hizo, Mhe. Limbe amesema Serikali inaendelea kuboresha sekta ya elimu kupitia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2023. Amesema Halmashauri imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia.
“Tunazo takwimu sahihi za mahitaji ya kila shule na tutaendelea kuboresha miundombinu kulingana na vipaumbele vilivyowekwa,” amesema.
Huduma za maji na barabara
Kwa upande wa huduma ya maji, Meneja wa RUWASA wilayani humo Dickson Kamazima, akizungumza kwa njia ya simu amesema kuwa mradi wa maji umefika katika vijiji vyote na hatua inayofuata ni kusambaza huduma hiyo katika vitongoji ambavyo bado havijafikiwa katika mwaka ujao wa fedha huku akiendelea kuwahimiza wananchi kuendelea kulipia ankara za maji ili kuwezesha uendelevu wa huduma hiyo na upanuzi wake.
Akizungumzia miundombinu ya barabara, Meneja wa TARURA, Ing. Eliya Mgaya, kwa nnia ya simu amesema barabara ya Ngundangali–Kakola kupitia Nida yenye urefu wa kilomita 7.1 tayari imefanyiwa upembuzi yakinifu na inasubiri kibali ili kuanza utekelezaji wa ujenzi wake.

Kuhusu umeme, Mhe. Limbe amesema Serikali inaendelea na mpango wa kusambaza umeme vijijini. Aidha, kuhusu changamoto ya mawasiliano ya simu, amesema suala la ukosefu wa minara katika baadhi ya maeneo atalifikisha kwenye mamlaka husika ili lipatiwe ufumbuzi na baadaye kutoa mrejesho kwa Diwani wa Kata.
Afisa Tarafa ya Kishapu Tano Malele
Diwani wa Kata ya Uchunga, Mhe. Lukas Manyegule, amemshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na wataalamu kwa kufika kijijini hapo kusikiliza na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili wananchi na kujionea hali halisi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“Wananchi wa Kata ya Uchunga wamekuwa na imani kubwa kwa Serikali yao. Ujio wa viongozi pamoja na wataalamu ni fursa muhimu ya kupata majibu ya changamoto zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi wetu,” amesema Mhe. Manyegule.
Kwa upande wao, wananchi wameeleza kuridhishwa na utaratibu wa viongozi kuwafuata katika maeneo yao na kusikiliza changamoto zao moja kwa moja wakiongeza kuwa ziara hiyo imewapa matumaini mapya ya kupatiwa ufumbuzi wa changamoto za muda mrefu katika sekta za afya, elimu, maji, mawasiliano na miundombinu ya barabara.
Mkazi wa Kijiji cha Unyanyembe, Happiness John, amesema upatikanaji wa huduma ya umeme katika vitongoji vilivyobaki utachochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi huku Moshi John ameomba Halmashauri kuharakisha ukarabati wa Shule ya Msingi Unyanyembe ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira salama na yenye viwango vinavyostahili.
Wananchi wengine wamempongeza Mhe. Limbe kwa kuahidi kuchangia maendeleo ya Zahanati ya Unyanyembe na kuahidi kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo kupitia nguvu kazi na michango yao ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii.
إرسال تعليق