Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe Josephat Limbe (kushoto) akikabidhi zawadi iliyotolewa na Jeshi la polisi wilayani humo kwa wahitimu wa Kidato Cha nne kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukenyenge Mwl. Majige Magembe (kulia)
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Josephat Limbe, amewashauri wakuu wa Shule wilayani humo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu maandalizi ya wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kitaifa, ili mabadiliko ya ratiba yasiiathiri ufaulu wao.
Mhe. Limbe ametoa ushauri huo akiwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 17 ya Shule ya Sekondari Ukenyenge, ambapo pia amewapongeza wanafunzi wanaohitimu kwa hatua hiyo na kuwataka kuendelea kuwa na nidhamu, bidii na kutumia elimu waliyoipata kwa manufaa yao na jamii.
Aidha, amewataka wanafunzi wanaoendelea na madarasa ya chini kuongeza bidii katika masomo, kuheshimu walimu na wazazi pamoja na kutumia muda wao vizuri ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ijayo.
Akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukenyenge, Mwl. Majige Magembe, amesema shule imeweka mikakati ya kuwaandaa wanafunzi kwa kutumia muda uliobaki, ikiwemo kuongeza msisitizo katika maeneo muhimu ya masomo na kuwahamasisha wanafunzi kuongeza bidii katika maandalizi ya mitihani.
Mwl. Magembe pia amewapongeza wahitimu kwa kukamilisha hatua hiyo ya elimu na kuwataka kuendelea kuthamini elimu, nidhamu na maadili waliyofundishwa shuleni.
Awali, Mtihani wa Kidato cha Nne ulikuwa umepangwa kuanza Novemba 3 mwaka huu, lakini Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limebadilisha ratiba hiyo na mtihani huo sasa unatarajiwa kuanza Oktoba 19.
Mabadiliko hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Ukenyenge, huku walimu wakieleza kuwa wataweka mikakati mbalimbali kuhakikisha muda uliobaki unatumiwa ipasavyo na mabadiliko hayo hayaathiri ufaulu.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukenyenge Mwl. Majige Magembe akizungumza kwenye mahafali hayo
Mabadiliko hayo yamepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Ukenyenge, huku walimu wakieleza kuwa wataweka mikakati mbalimbali kuhakikisha muda uliobaki unatumiwa ipasavyo na mabadiliko hayo hayaathiri ufaulu.
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ukenyenge Mwl. Majige Magembe akizungumza kwenye mahafali hayo







Post a Comment