Picha na Marco Maduhu
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umewataka wanachama na wastaafu kutumia mifumo rasmi ya kidijitali kuhakiki taarifa za michango na mafao yao, huku wakionya dhidi ya watu wanaojitambulisha kama mawakala wa mfuko huo.
Wito huo umetolewa leo, Septemba 18, 2026, mjini Shinyanga wakati wa semina ya PSSSF kwa waandishi wa habari kutoka Shinyanga na Simiyu pamoja na Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN).
Afisa Msimamizi wa PSSSF Mkoa wa Simiyu, Salum Mwegelo, amesema baadhi ya wastaafu wamekuwa wakilengwa na watu wanaodai wanaweza kuwasaidia kufuatilia mafao, huku wakiwaomba taarifa za siri za akaunti zao.
Amesema PSSSF haina mawakala wanaotoa huduma kwa niaba ya mfuko huo, hivyo wanachama na wastaafu wanapaswa kutumia njia rasmi na kutompa mtu mwingine namba za siri au taarifa zao za kifedha.
“Mawakala hao huwarubuni wastaafu na kuomba namba za siri na taarifa muhimu, ikiwemo taarifa za akaunti zao, na kisha kuzitumia kufanya miamala bila ridhaa ya wahusika,” amesema Mwegelo.
Ameongeza kuwa mifumo ya kidijitali inamwezesha mwanachama kufuatilia taarifa za michango na mafao yake na kubaini mapema taarifa zisizo sahihi kabla ya kufikia hatua ya kudai mafao.
Naye Kaimu Afisa Mfawidhi PSSSF Shinyanga, Sunday Rashid, amesema mfuko huo umeanza kushughulikia taarifa za watumishi wanaokaribia kustaafu miezi sita kabla ya tarehe rasmi ya kustaafu, ili kutoa muda wa kuhakiki taarifa na kurekebisha changamoto zinazoweza kujitokeza.
Kwa upande wake, Mratibu wa TBN Kanda ya Ziwa, Kadama Malunde, amewataka waandishi kutumia taaluma yao kuwaelimisha wananchi kuhusu haki na huduma za hifadhi ya jamii.
“Kwa mwandishi wa habari, kujifunza ni sehemu ya kazi yetu. Dunia inabadilika, teknolojia inabadilika na mahitaji ya jamii yanabadilika,” amesema Malunde.
Amesema waandishi wanapaswa kuhakikisha taarifa wanazowafikishia wananchi zinathibitishwa, zina usahihi na zinatoka katika vyanzo vinavyoaminika.
Semina hiyo imelenga kuongeza uelewa wa waandishi kuhusu huduma za PSSSF, matumizi ya mifumo ya kidijitali, haki na wajibu wa wanachama pamoja na namna ya kujikinga na utapeli.

Afisa Uhusiano kutoka PSSSF Abdul Njaidi akizungumza katika mafunzo hayo.

Afisa Mahusiano na Mtoa elimu kwa wanachama PSSSF Flora Sumari, akizungumza katika mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Post a Comment