KAMATI YA BUNGE YAKAGUA UZALISHAJI WA DAWA ZA ASILI DAR ES SALAAM

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI leo Oktoba 25, 2026, imetembelea kiwanda cha kutengeneza dawa za asili jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na maendeleo ya uwekezaji katika eneo hilo.



Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wawekezaji pamoja na wadau wa tiba asili katika kuimarisha utoaji wa huduma za afya nchini.


Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo kwa kuzingatia ubora, usalama na ufanisi wa dawa za asili ili kuhakikisha zinachangia katika kuboresha huduma za afya kwa Watanzania.
















0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم