Na Sumai Salum-Kishapu
Kampeni ya chanjo ya polio awamu ya pili imezinduliwa rasmi Mei 4, 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kutokomeza kabisa maambukizi ya ugonjwa huo nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe wilayani humo, Dkt. Joseph Bahati, amesema mpango huo wa Serikali kupitia Wizara ya Afya unalenga kuimarisha kinga na kuzuia maambukizi ya magonjwa kwa njia ya chanjo, hivyo ni muhimu kwa jamii kushiriki kikamilifu.
Dkt. Bahati, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza uelewa kuhusu chanjo hiyo. Ameeleza kuwa chanjo zimechangia kwa kiwango kikubwa kupunguza maambukizi ya magonjwa mbalimbali ambayo hapo awali yalikuwa tishio kwa taifa.
Aidha, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa juhudi zake za kulinda afya ya jamii, na kuwashukuru wadau wote wanaoendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa majukumu hayo muhimu.
Kwa upande wake, Msimamizi wa Uhamasishaji wa Chanjo ya Polio kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Matilda Halamga, amepongeza mafanikio ya awamu ya kwanza ya kampeni hiyo kwa Wilaya ya Kishapu na kuhimiza kuongeza juhudi zaidi katika awamu ya pili ili kuhakikisha kila mtoto anafikiwa na chanjo hiyo.
Akiwasilisha mada kuhusu chanjo ya matone ya polio aina ya nOPV2, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoa wa Shinyanga, Moses Mwita, amesema lengo la kampeni hiyo ni kuimarisha kinga, kuzuia kusambaa kwa virusi vya polio, na kulinda watoto dhidi ya ulemavu wa kudumu.
Mwita ameongeza kuwa ni muhimu kwa jamii kutambua dalili za ugonjwa wa polio, zikiwemo kulegea kwa viungo, kupoteza nguvu za mwili, kushindwa kutembea na ulemavu wa ghafla, huku akisisitiza kuwa watoto wote wanapaswa kupata chanjo hiyo kwa wakati.
Msimamizi wa zoezi la chanjo ngazi ya Mkoa, Halima Hamisi, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa wadau wote ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa na kufikia watoto wote waliolengwa wenye umri wa chini ya miaka kumi.
Kwa pamoja, washiriki wa uzinduzi huo wameahidi kushirikiana kikamilifu kwa kutumia majukwaa yao katika kuhamasisha jamii ili kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo na hivyo kuendelea kulinda afya ya jamii dhidi ya ugonjwa wa polio.
Ikumbukwe kuwa mpango wa Taifa wa chanjo ulianzishwa mwaka 1975,huku mwaka 1996 iliripotiwa kesi moja ya polio nchini, hakuna mgonjwa mwingine aliyebainikana sasa juhudi hizi zinaendelea kufuatia kubainika kwa vimelea vya virusi vya polio katika majitaka mkoani Mwanza
Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo, viongozi wa dini, walimu wa shule za msingi, waratibu elimu, watalamu wa tiba za asili, wazee maarufu, wamiliki na viongozi wa shule binafsi za kutwa na Sungusungu huku awamu hii ya pili itaendelea kutekelezwa kwenye Mikoa ya Shinyanga, Mara, Mwanza, Kagera, Simiyu, Geita, Singida na Tabora.
Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Dkt. Joseph Bahati akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanjo ya polio awamu ya pili kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Mei,4,2026 katika ukumbi wa hospital ya Wilaya ya Dkt. Jakaya Kikwete 
Msimamizi wa uhamasishaji wa Chanjo ya Polio kutoka Wizara ya Afya Dkt. Matilda Halamga akizungumza kwenye kikao Cha uzinduzi wa Chanjo ya Polio awamu ya pili wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kwenye ukumbi wa hospital ya Dkt. Jakaya Kikwete Mei, 4, 2026 Msimamizi wa Chanjo
إرسال تعليق