Mkoa wa Singida unatarajiwa kuwa mwenyeji wa moja ya matukio makubwa ya kijamii na maendeleo mwaka 2026 kupitia hafla ya Usiku wa Wadau Shupavu na Tuzo za Mdau Shupavu – Mkoa wa Singida 2026, tukio litakalowakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo, wafanyabiashara, viongozi, vijana, wasanii pamoja na taasisi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Singida.Tukio hilo linaandaliwa na Taasisi ya HolySmile, ikiongozwa na Mkurugenzi wake, Arnold Bweichum,. Kwa mujibu wa waandaaji, hafla hiyo kubwa itakayofanyika Mei 25, 2026 katika ukumbi wa Aqua Hall uliopo Singida Manispaa huku ikitarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya wageni kutoka sekta mbalimbali za maendeleo ndani ya Mkoa wa Singida na maeneo mengine ya Tanzania.
Waandaaji wameeleza kuwa MDAU SHUPAVU AWARDS 2026 sio tukio la kawaida la utoaji wa tuzo pekee, bali ni jukwaa maalum la kuunganisha wadau kutoka sekta mbalimbali kwa lengo la kujenga ushirikiano, kupanua mtandao wa kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha maendeleo endelevu ndani ya Mkoa wa Singida.
Kupitia mandhari isemayo “Kuunganisha Wadau, Kuendeleza Maendeleo”, hafla hiyo inalenga kuimarisha mshikamano wa kijamii na kibiashara pamoja na kutoa motisha kwa watu na taasisi zinazofanya kazi kubwa katika jamii.
Aidha, waandaaji wamebainisha kuwa tukio hilo litatoa nafasi kwa wadau mbalimbali kubadilishana uzoefu, kujifunza fursa mpya za maendeleo pamoja na kujenga mahusiano yatakayosaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Tuzo za Mdau Shupavu zilianzishwa mwaka 2022 katika Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuwatambua wadau waliokuwa wakifanya kazi kubwa za maendeleo katika jamii. Kufuatia mafanikio makubwa ya mashindano hayo, mfumo huo ulipanuka katika mikoa mbalimbali nchini mwaka 2023 na 2024.
Mwaka 2025, Taasisi ya HolySmile ilipanua mfumo huo hadi ngazi ya Kanda ya Ziwa kwa kushirikisha mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Simiyu, Mara, Kagera, Kigoma, Tabora pamoja na Singida.
Kwa mwaka 2026, Mkoa wa Singida unaendelea kuwa sehemu muhimu ya mfumo huo ambapo washindi wa vipengele mbalimbali watapata nafasi ya kuwakilisha mkoa katika mashindano ya ngazi ya kanda na baadaye kitaifa.
Aidha Washiriki watashindanishwa katika vipengele mbalimbali vinavyogusa sekta tofauti za jamii ikiwemo sanaa, michezo, biashara, habari, urembo, ubunifu pamoja na huduma za kijamii.
Best Male MCBest Female MCBest DJBest Sports PersonalityBest Entrepreneur / Business LeaderBest Innovative Business / CompanyBest PhotographerBest VideographerBest Blogger / Online News PortalBest Social Media InfluencerBest Community Development GroupBest Tourism Influencer
Washindi wa vipengele hivyo watapatikana kupitia mfumo wa kura za umma kwa asilimia 70 pamoja na tathmini ya majaji wa kitaalamu kwa asilimia 30.
Aina za Tuzo Zitakazotolewa
Waandaaji wameeleza kuwa kutakuwa na aina tatu za tuzo ambazo ni:
1. Tuzo za Ushindani
Tuzo zinazotolewa kwa washiriki wanaoshindanishwa rasmi kupitia kura za umma pamoja na tathmini ya majaji wa kitaalamu.
2. Tuzo za Heshima
Tuzo maalum zitakazotolewa kwa watu au taasisi zilizotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii bila kupitia ushindani wa kawaida.
Tuzo zitakazotolewa kwa washiriki au taasisi zenye mafanikio yanayoweza kupimika kupitia takwimu na matokeo ya kazi zao.
Washindi na Runners Up Kutambuliwa Rasmi
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya waandaaji, washindi wote pamoja na washindi wa pili (Runners Up) watatambuliwa rasmi jukwaani na kukabidhiwa vyeti vya ushindi na ushiriki siku hiyo hiyo ya hafla.
Vyeti na tuzo zitatolewa papo kwa papo mbele ya wageni wote watakaohudhuria tukio hilo, jambo linalolenga kuongeza thamani na heshima kwa washiriki wote wa mashindano hayo.

Post a Comment