DAS FATMA: MWENGE NI ALAMA MUHIMU YA TAIFA








Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Fatma Mohamed akizungumza

Na Sumai Salum – Kishapu

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Fatma Mohamed, amewahimiza wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru, unaotarajiwa kuwasili wilayani humo mnamo Agosti 18, 2026.

Fatma ametoa hamasa hiyo Jumamosi, Agosti 1, 2026, wakati akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, katika shughuli ya 'jogging' iliyolenga kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.

Amesema Mwenge wa Uhuru ni alama muhimu ya Taifa inayobeba ujumbe wa amani, umoja, mshikamano na maendeleo, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kuupokea na kushiriki katika shughuli mbalimbali utakapowasili wilayani humo.

Ikumbukwe kuwa kauli mbiu ya Mwenge 2026 "Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo" wakiongozwa na mkimbiza Mwenge kitaifa Ndg. Wazo Michael






















































0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post