Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo Kishapu Fabian Makongo akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Na Sumai Salum-Kishapu
-Tarura Kishapu Yatenga Milion 40 kukarabati barabara ya Isoso-Mwabusiga
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga umetenga Sh. milioni 40 kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Isoso–Mwabusiga, huku ukiahidi kufanya maboresho katika barabara nyingine korofi ili kupunguza changamoto za usafiri, hasa wakati wa msimu wa mvua.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Hussein Shaweji, Oktoba 26, 2026, wakati akijibu hoja za madiwani wa Kishapu (Mhe. Joel Ndettoson) na Mwataga (Mhe. Daudi Matungwa) katika mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, uliojikita katika kujadili taarifa za utekelezaji wa kamati kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, kuanzia Julai hadi Septemba.
Akijibu hoja ya Diwani wa Kata ya Kishapu, Joel Ndettoson, kuhusu mpango wa ukarabati wa barabara ya Isoso–Mwabusiga, Shaweji amesema fedha za Sh milioni 40 tayari zimetengwa na TARURA inasubiri kupokea fedha hizo ili kuanza kazi.
“Kuhusu barabara ya Mhunze–Mwamagembe, napenda kukiri kuwa kweli inahitaji ukarabati na tayari tumeshatoa taarifa kuhusu changamoto hiyo. Pia, barabara ya Isoso–Migunga yenye urefu wa kilomita mbili itafanyiwa maboresho kwa kuweka vifusi katika maeneo korofi ili kupunguza changamoto kwa wananchi wakati wa msimu wa mvua,” amesema Shaweji.
Akijibu swali la Diwani wa Kata ya Mwataga, Daudi Matungwa, aliyehoji hatua zinazochukuliwa kukarabati barabara ya Mhunze–Mwamagembe, ambayo imekuwa na changamoto za kupitika, hususan wakati wa mvua, Shaweji amesema kuwa TARURA inapanga kuboresha barabara kadhaa ndani ya Mji Mdogo wa Kishapu kwa kuziweka katika kiwango cha changalawe, kujenga mitaro ya kupitisha maji na kufunga taa za barabarani katika maeneo yaliyopangwa. Barabara hizo ni Ded–DC yenye urefu wa kilomita mbili, RC kilomita 1.7, Vicky kilomita 0.3, Shapu, Omary, Bujilima na barabara ya eneo la mnadani hadi kwa Mabela.
Amefafanua kuwa maboresho hayo yatajumuisha uwekaji wa changarawe katika barabara husika, ujenzi wa mitaro katika maeneo yaliyopangwa na uwekaji wa taa za barabarani katika barabara za Ded–DC na Bujilima, pamoja na barabara ya mnadani hadi kwa Mabela.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, Fabiani Makongo, amewataka viongozi wa vitongoji kutekeleza majukumu yao kwa vitendo badala ya kulalamika, huku akiwataka kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha hayatoroshwi kupitia shughuli za biashara ya madini ya ujenzi na mazao katika maeneo yao.
Makongo pia amemshauri Afisa Biashara kushirikiana na viongozi wa mamlaka hiyo kuwafikia wamiliki wa baa zinazotoa huduma za muziki na kuwapatia miongozo ya kiutendaji, ili biashara hizo ziendeshwe kwa kuzingatia taratibu na kulinda usalama na ustawi wa jamii inayozizunguka.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ambaye pia ni Afisa Tarafa ya Kishapu, Tano Malele, amewataka viongozi kuepuka kuwa chanzo cha migogoro katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, na kuhakikisha wanafunzi wanapata haki yao ya kusoma huku wakishirikiana kupinga ndoa za utotoni.
“Niwaombe pia maafisa wa Ardhi na Mipango Miji wawafikie wananchi na kuwapa elimu kuhusu kuzingatia mipaka na hifadhi za barabara, ili wanapopanga na kutekeleza shughuli zao za uwekezaji wasivamie maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya barabara,” amesema Malele.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Niceforus Mgaya, amewataka viongozi kudumisha umoja, ushirikiano na kuheshimiana katika utekelezaji wa majukumu yao, akisisitiza umuhimu wa ubunifu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vilivyopo.
“Nimeletwa Kishapu na Mheshimiwa Rais ili tushirikiane nanyi kufanya kazi kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi. Hivyo, tunapaswa kuwa wamoja na kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na watangulizi wetu, huku tukijitahidi kufanya vizuri zaidi ili wananchi waendelee kunufaika na kazi zetu,” amesema Mgaya.
Katika mkutano huo, wajumbe pia wameelekeza usimamizi wa kivuko kilichojengwa katika eneo la Hoteli ya Jiganga, ambacho kilielezwa kutofuata taratibu zinazotakiwa na kuzuia maji kutiririka kwa uhuru, hali inayosababisha maji kutuama na kuhatarisha usalama wa watoto na wakazi wa maeneo jirani.
Baraza limemshauri Afisa Mazingira kusimamia suala hilo kwa mujibu wa taratibu na sheria, ikiwemo kuchukua hatua zinazostahili kuhusu kivuko hicho ili kurejesha mtiririko wa maji na kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza.
Aidha Baraza hilo limepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, pamoja na taarifa za kamati za kudumu za Halmashauri, ambazo ni Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Uchumi, Mazingira na Mipango Miji, na Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango.
Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu ina jumla ya kata mbili, ambazo ni Kishapu na Mwataga, zenye vitongoji 11.
Mtendaji wa mamlaka ya Mji mdogo Kishapu Godwin Everygist Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, akizungungumza kwenye mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Mwakilishi wa Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambaye ambaye pia ni Afisa Tarafa ya Kishapu Tano Malele, akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Niceforus Mgaya, akizungumza wakati mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Makamo Mwenyekiti wa baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu Mkoani Shinyanga Dionis Makala akizungungumza kwenye mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Elizaberth Sonda akiwasilisha taarifa ya kamati ya Huduma ya jamii
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Mazingira na Mipango Miji Charles Mbugangali akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo
Makamo Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo Dionis Makala akiwasilish taarifa ya kamati ya Fedha Utawala na Mipango kwa niaba ya Mwenyekiti wa Baraza hilo
Mwakilishi wa Meneja wa TARURA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Hussein Shaweji akizungungumza kwenye kikao cha Baraza la mamlaka ya mji mdogo Kishapu uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Diwani wa Kata ya Kishapu Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Diwani wa Kata ya Mwataga Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Daudi Matungwa, akichangia hoja wakati wa mkutano wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kishapu, uliofanyika Oktoba 26, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, wenye lengo Kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za kudumu za Halmashauri na vitongoji kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027 Julai–Septemba
Post a Comment