
Meya wa Jiji la Mwana na Mwenyekiti mpya ALAT Taifa, akipokea zawadi kutoka kwa Meneja PSSSF Kanda ya Ziwa Mashariki, CPA Rajabu Kinande alipotembelea huduma za PSSSF zinazoendelea kutolewa katika maonyesho yanayofanyika sambamba na Mkutano Mkuu wa 40 ALAT
Bi. Glory Selene Chidumizi, Afisa Huduma Kwa Wateja wa PSSSF Makao Makuu, akimuhudumia mwanachama wa Mfuko Bi. Diana Zacharia Sonno, katika maonyesho yanayoendelea sambamba na mkutano mkuu wa ALAT
Bi. Aziza Baruti Mkurugenzi Halmashauri ya Butiama, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea huduma za PSSSF zinazoendelea kutolewa katika maonyesho yanayofanyika sambamba na Kikao kikuu cha ALAT jijini Mwanza.

Mhe. Isack Joseph Copriano, Mbunge wa Monduli (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa PSSSF mara baada ya kutembelea banda la PSSSF katika maonyesho yanayofanyika sambamba na kikao cha 40 cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT)
Meneja wa kanda ya Ziwa Mashariki CPA. Rajabu Kinande wakiwa na Afisa wa PSSSF Bw.Nyanga M . Makani wakufatilia ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 40 wa ALAT uliofunguliwa leo na Mh. Mwigulu Nchemba jijini MwanzaMwanza, Novemba 16, 2026
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika maonesho yanayoambatana na Mkutano Mkuu wa 40 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), yanayofanyika jijini Mwanza.
Mkutano huo umefunguliwa rasmi Novemba 16, 2026, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, na unatarajiwa kuhitimishwa Novemba 20, 2026.
Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika maonesho hayo, Meneja wa Kanda ya Ziwa Mashariki wa PSSSF, CPA Rajab Kinande, amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa Mfuko kukutana na wadau wake, hususan watumishi wa Serikali za Mitaa, ambao ni miongoni mwa wanachama wake.
Amesema kupitia maonesho hayo, watumishi hao watapata fursa ya kufahamu majukumu ya Mfuko, huduma zinazotolewa pamoja na maboresho mbalimbali yaliyofanyika kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu na hatimaye kufikia lengo kama kauli mbiu isemavyo ‘tunalipa jana’
Aidha, amesema ushiriki wa PSSSF katika maonesho hayo ni sehemu ya jitihada za Mfuko za kusogeza huduma karibu na wanachama wake, kuwaelimisha kuhusu haki na stahiki zao pamoja na kuwajengea uelewa wa namna bora ya kutumia mifumo ya kidijitali inayowezesha upatikanaji wa huduma kwa urahisi na haraka.
Mwisho.
Post a Comment