Chanzo cha picha,EPA
N
Rais Donald Trump wa Marekani amesema hakuna shaka kwamba Marekani imepata "ushindi kamili" baada ya kukubaliana kuhusu kusitisha vita kwa wiki mbili na Iran.
Katika mahojiano na Agence France Presse baada ya tangazo lake, alisema kwamba urani iliyorutubishwa ya Iran "itajadiliwa kikamilifu" chini ya makubaliano hayo.
"Vinginevyo nisingekubali," Trump alisema, bila kutoa maelezo yoyote kuhusu kile ambacho kingetokea kwa Iran.
Alipoulizwa kama angerudi kutoa tena vitisho kama vya awali vya kuharibu mitambo ya nishati na madaraja ya Iran ikiwa makubaliano hayo yangevunjika, alichosema tu ni: "Utalazimika kufuatilia hili."
Trump, ambaye anatarajiwa kusafiri hadi China mwezi ujao kukutana na mwenzake wa China Xi Jinping, alisema: "Nasikia hivyo" alipoulizwa kama Beijing ilihusika katika kumfanya mshirika wake mkuu Tehran kujadiliana kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano.

IRAN
Wakati huohuo Serikali ya Iran na vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema kuwa makubaliano ya kusitisha mashambulizi kwa muda ni ushindi mkubwa kwa utawala wa taifa hilo.
Katika taarifa iliyotolewa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, Iran imesema imeafikia karibu malengo yake yote ya vita hivyo na kuwa adui wake amepata pigo la kihistoria.

Chanzo cha picha, Reuters
Ikumbukwe kwamba vita hivyo vilianza na kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa taifa hilo Ali Khamenei na viongozi wengine wakuu wakijeshi na hii ilikuwa tishio kubwa kwa utawala wa Iran.
Iran inajiona mshindi kwa kuweza kustahimili vita vilivyoanzishwa na Israel na Marekani kwa zaidi ya siku 30.
Post a Comment