RC MHITA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA BABA WA MKUU WA WILAYA YA KISHAPU


Na Sumai Salum- Mwanza


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameongoza mamia ya watu walioshiriki mazishi ya baba mzazi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Nicholaus Masindi. Mazishi hayo yamefanyika katika makabuli ya familia, Kijiji cha Ngoma 'B' Kata ya Nyamatongo, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Juni 19,2026.


Akizungumza wakati wa mazishi, Mhe. Mhita amesema kifo ni funzo kwa wanadamu wote kutambua Kila mmoja anao mwisho wake wa kuishi hapa duniani hivyo wanapaswa kutenda mema, kuishi kwa upendo, kushirikiana na kuwajali wengine katika jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita

Mhe. Mhita ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, akieleza kuwa historia ya marehemu imeonesha alifanya kazi kubwa katika kutunza familia yake, kuwekeza na kudumisha mahusiano mazuri na jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Nicholaus Masindi

Mzee Nicholaus Masindi alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 92. Familia yake imetoa shukrani kwa wote walioshiriki kwa hali na mali katika safari ya mwisho ya mpendwa wao aliyefariki Juni 15, 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Geita Mhe. Martin Shigela
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Mhe. Frenk Nkinda
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza Mhe. Johari Samizi
Katibu Tawala Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson
Tazama picha za matukio mbalimbali






































































































































































































0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post