SHAGY ACADEMY KUCHUANA NA BIASHARA UTD NZEGA

Kikosi cha SHAGY ACADEMY kutoka Sikonge mkoani Tabora, Jumamosi hii Mei 9, 2026 kitasafiri kuelekea Zenga kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya BIASHARA UTD utakaopigwa Jumapili Mei 10, 2026 katika Uwanja wa Samora.


Wadau wa michezo na wapenda soka mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vya vijana wa SHAGY ACADEMY wakionyesha uwezo wao dimbani katika mchezo huo wa kuvutia.

Aidha, waandaaji wametangaza kuwa mchezo wa fainali ya SHAGY CUP kati ya MASENARIES dhidi ya MWANAGWALELA wilayani Kishapu mkoani Shinyanga unatarajiwa kupigwa mwezi Julai mwaka huu.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post