Baada ya kugusa mioyo ya waumini na wapenzi wa muziki wa Injili kupitia wimbo "Tuimbe Tumepona" aliomshirikisha Mwinjilisti Daniel Safari, msanii wa nyimbo za Injili Jesca Simuchile amerejea na kazi mpya yenye ujumbe mzito wa matumaini na imani kwa Mungu, "Neema Ingalipo".Katika wimbo huu mpya, Jesca anaimba kwa lugha ya Kiswahili huku akisisitiza kuwa neema ya Mungu bado ipo na inatosha kubadilisha maisha ya kila anayemwamini na kumtumainia Mungu.
Kinachoufanya mradi huu kuwa wa kipekee ni kwamba video yake rasmi imeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu (4K) na imewekewa tafsiri za lugha ya Kiingereza (English subtitles), hatua inayowawezesha watazamaji wasioweza kuzungumza Kiswahili kuelewa kwa urahisi ujumbe unaobebwa na wimbo huo.
Kupitia ubunifu huo, Jesca Simuchile anaendeleza dhamira yake ya kuifikisha Injili kwa watu wa mataifa mbalimbali, akitumia muziki wa Kiswahili kama chombo cha kuhubiri huku akivuka mipaka ya lugha kupitia tafsiri ya Kiingereza.
Wimbo huo umebeba mashairi yenye kugusa moyo, sauti ya kuvutia na picha zenye ubora wa hali ya juu, ukitoa ujumbe wa faraja, matumaini na kumtegemea Mungu katika kila hali ya maisha.
Jesca anawaalika waumini na wapenzi wa muziki wa Injili kutazama video rasmi ya "Neema Ingalipo", kushiriki ujumbe huo kwa wengine na kuendelea kumuunga mkono kwa kujisajili kwenye chaneli yake ya YouTube ili kupata kazi zake mpya.
Tazama hapa video ya Jesca Simuchile - Neema Ingalipo
إرسال تعليق