.jpeg)
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri ya ADEM, Dkt. Hillary A. Dachi, amewasili rasmi chuoni hapo na kuongoza kikao chake cha kwanza tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, ambapo Bodi ilikutana kujadili masuala mbalimbali ya kimkakati yanayolenga kuimarisha utendaji wa taasisi na kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Kikao hicho, ambacho ni Kikao cha 62 cha Bodi ya Ushauri ya ADEM, kilifanyika katika Kampasi ya Bagamoyo na kuhudhuriwa na wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti ya taasisi wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid J. Maulid.
Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Dachi alieleza dhamira yake ya kushirikiana kwa karibu na wajumbe wa bodi pamoja na menejimenti ya ADEM ili kuhakikisha taasisi inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, ubunifu na weledi mkubwa katika kuandaa na kuendeleza viongozi wa elimu wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za wakati.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid J. Maulid, alimkaribisha rasmi Mwenyekiti huyo mpya na kumhakikishia ushirikiano wa karibu kutoka kwa menejimenti na watumishi wa taasisi katika kutekeleza maamuzi na maelekezo yatakayosaidia kuifikisha ADEM katika viwango vya juu zaidi vya utoaji huduma.
Katika kikao hicho, wajumbe wa bodi walipata fursa ya kujadili na kutoa maelekezo kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya taasisi, ikiwemo utekelezaji wa mipango ya kimkakati, ubora wa mafunzo, uendelevu wa programu za kitaaluma pamoja na fursa za kukuza mchango wa ADEM katika maendeleo ya sekta ya elimu na Taifa kwa ujumla.
Kikao cha 62 cha Bodi ya Ushauri ya ADEM kinaashiria mwanzo wa hatua mpya ya kuimarisha usimamizi na uongozi wa taasisi hiyo, huku kikidhihirisha dhamira ya viongozi wake kuendelea kuifanya ADEM kuwa kitovu cha ubora katika maendeleo ya uongozi na usimamizi wa elimu nchini Tanzania.
.jpeg)
.jpeg)





.jpeg)






Post a Comment