SPIKA WA BUNGE ATEMBELEA NA KUKAGUA SHULE YA MFANO YA BENKI YA CRDB

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mussa Azan Zungu ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mfano ya Benki ya CRDB (CRDB Bank Secondary Model School) inayojengwa Upanga Halmashauri ya Ilala mkoani Dar salam.



Mhe. Zungu amepokelewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, TullyEsther Mwambapa huku akipongeza kasi ya mkandarasi na kumuhimiza akamilishe ujenzi mapema iwezekanavyo ili kuwanufaisha wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga.


"Shule hii inajengwa Ilala ila itawahudumia wanafunzi kutoka kila maeneo mengi ya ndani na nje ya Tanzania, hivyo Nampongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid Nsekela na menejimenti nzima kwa kuona umuhimu wa kujenga shule hii itakayowafaa hasa kwanza watoto wa Kitanzania. Nikuombe mkandarasi, ongeza kasi ujenzi ukamilike mapema," amesema Spika Zungu.


Akieleza maendeleo ya mradi huo, Tully amesema mradi huo utakagharimu jumla ya shilingi bilioni 5. "Itakuwa shule bora na ya kisasa. Tunashukuru serikali ya Manispaa ya Ilala kwa kutuamini na kushirikiana nasi kuboresha maisha ya wananchi," amesema Tully.


Kuhusu kukamilika kwa ujenzi huo,mkandarasi wa mradi huo, Mhandisi Anna Mafoka, amesema mkataba ulitaka shule hiyo ijengwe kwa miezi 10 na kukamilika Machi 2027 lakini watajitahidi ifikapo Januari 2027 yaanze kutumika.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post