Wakimbizi wapatao 155,811 wanaohifadhiwa katika maeneo mbalimbali nchini wameiomba Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na wananchi wote kuendelea kulinda amani iliyopo, wakibainisha kuwa kukosekana kwa amani kunasababisha watu kupoteza kila kitu na kulazimika kukimbilia nchi nyingine na kwamba yaliyowakuta wao ni mfano hai.
Wakimbizi hao wametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Juni, yakiwa na kaulimbiu isemayo “Hadi Kila Mtu Awe Salama”.
Walitoa shukrani za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan, na wananchi kwa ujumla kwa kuendelea kuwapa hifadhi na usalama bila ubaguzi.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Tanzania inapaswa kujifunza kutokana na hali zilizotokea katika nchi jirani na kuendelea kuimarisha mazingira ya amani na utulivu.
Amesema serikali itaendelea kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini na kuhakikisha usalama wao, huku akisisitiza kuwa amani ni msingi muhimu unaowezesha wananchi kujikita katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi.
Alieleza kuwa ni agizo la Rais Samia kuwa serikali itaendelea kuwahudumia wakimbizi wote waliopo nchini kwa kuzingatia utu na haki za binadamu.
Alikumbusha kuwa msimamo wa Tanzania kwa sasa ni kuhimiza urejeaji wa hiari wa wakimbizi kwenda maeneo salama kama suluhisho bora zaidi.

Post a Comment