WAZIRI MKUU ATOA TSH MILIONI 20 KUUNGA MKONO SACOSS YA BODABODA MBEYA


Na Godfrey Mushi


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameahidi kutoa shilingi milioni 20 kuunga mkono uanzishaji wa SACOSS ya waendesha bodaboda wa Jiji la Mbeya.


Ahadi hiyo imetolewa kupitia simu wakati wa mkutano ulioandaliwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Patrick Mwalunenge, uliowakutanisha waendesha bodaboda kujadili fursa za kuanzisha mfuko wao wa ushirika wa akiba na mikopo.


Hatua hiyo inalenga kuwawezesha bodaboda kujenga mtaji wao wenyewe, kupata mikopo nafuu na kuwekeza katika miradi ya maendeleo itakayoboresha maisha yao na familia zao.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post