Shule za msingi na sekondari Tarafa ya Mondo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga zimekutana katika bonanza la michezo lililolenga kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi, hususan mchezo wa netiboli katika ngazi za shule za msingi na sekondari Julai 31, 2026 viwanja vya michezo shule ya Msingi Ng'wanima lililoandaliwa na Walimu wa michezo wa shule hizo.Bonanza hilo lilihusisha michezo ya mpira wa Pete na mpira wa miguu, huku shule mbalimbali zikishindana kuonesha uwezo wao. Katika mchezo wa pete, Shule ya Msingi Buchambi imeibuka mshindi, wakati Shule ya Msingi Ng’wanima ikitwaa ubingwa wa mpira wa miguu.
Bonanza hilo limeshirikisha jumla ya shule nane ambazo ni Ng’wanima Primary, Busangwa Primary, Ng’wajipugila Primary, Mwigumbi Primary, Buchambi Primary, Bubiki Primary, Bunambiyu Sekondari na Ng’wanima Sekondari.






إرسال تعليق