KISIMA MAJABALA AKUTANA NA MKUU WA WILAYA YA KISHAPU KUJADILI BURUDANI YA MWENGE WA UHURU 2026


Mwanamuziki wa nyimbo za asili ya Kisukuma, Kisima Majabala, amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, kwa ajili ya kujadili maandalizi ya burudani itakayopamba mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zitakapowasili wilayani Kishapu.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, amesema wilaya hiyo imejipanga kikamilifu kuhakikisha Mwenge wa Uhuru unapokelewa kwa mafanikio makubwa, huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki shughuli zote zilizopangwa.

"Tunawakaribisha wananchi wote wa Kishapu na maeneo jirani kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika Agosti 18, 2026. Siku hiyo kutakuwa na uzinduzi wa miradi ya maendeleo, uwekaji wa mawe ya msingi, ukaguzi wa miradi mbalimbali pamoja na burudani ya kuvutia itakayotolewa na wasanii wetu wa asili," amesema Mhe. Masindi.

Kwa upande wake, Kisima Majabala amesema anajivunia kupata nafasi ya kushiriki katika burudani ya Mwenge wa Uhuru, akiahidi kuwapa wananchi wa Kishapu onyesho la kipekee litakaloendana na hadhi ya tukio hilo la kitaifa.

"Ni heshima kubwa kwangu kushiriki katika burudani ya Mwenge wa Uhuru. Nawashukuru viongozi wa Wilaya ya Kishapu kwa kuniamini, na nawaahidi wananchi burudani bora kupitia muziki wa asili ya Kisukuma," amesema Kisima Majabala.

Mwenge wa Uhuru 2026 unatarajiwa kuwasili Wilaya ya Kishapu mnamo Agosti 18, 2026, ambapo utakagua miradi ya maendeleo, kuzindua miradi mbalimbali na kuweka mawe ya msingi katika miradi inayoendelea kutekelezwa wilayani humo.

Wakati huo huo, Kisima Majabala anatarajiwa kufanya onyesho maalum la muziki jioni ya leo, Julai 17, 2026, katika Uwanja wa Mnadani, Mhunze, na kuwaalika mashabiki na wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi
Muimbaji wa nyimbo za asili ya kisukuma kutokea nchini Tanzania Kisima Majabala
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed
Diwani wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga mhe. Joel Ndettoson


























0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post