NDC YAAHIDI KUENDELEA KUTOA MAFUNZO YA KIMKAKATI YA ULINZI NA USALAMA


Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kimesema kitaendelea kutoa mafunzo ya kimkakati ya ulinzi na usalama ili kulinda amani na usalama wa nchi, huku kikieleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2011 chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Kauli hiyo imetolewa 
 Makao Makuu ya chuo hicho kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam na Mkuu wa chuo, Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, wakati wa mahafali ya Kozi ya 14 yaliyowahusisha maofisa waandamizi kutoka taasisi mbalimbali za serikali, wakala, na mataifa 16 rafiki ikiwa ni pamoja na Zambia, Ethiopia, Namibia, Kenya, Bangladesh na Misri.

Balozi Ibuge amebainisha kuwa washiriki wote wa ngazi ya Stashahada na Shahada ya Uzamili katika mafunzo hayo ya miezi 11 walifaulu vizuri kozi zao za kimkakati na ulinzi kwa kina, akisema mafanikio hayo yanatokana na usimamizi mzuri wa viongozi wakuu wa nchi.

Ametoa shukrani za pekee kwa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda, pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi kwa ushirikiano wao mkubwa na uongozi thabiti kwa ustawi wa chuo hicho.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post