DIWANI MAGANZO ATOA WITO WA UPENDO, UMOJA NA AMANI KATIKA KUFUNGA MAKAMBI JUMUISHI 2026


Diwani wa Kata ya Maganzo, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Hamza Tandiko, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha upendo, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi, akieleza kuwa misingi hiyo ni nguzo muhimu katika kuimarisha amani na utulivu nchini Tanzania.

Mhe. Tandiko ameyasema hayo Agosti 1, 2026, wakati akishiriki hafla ya kufunga Makambi Jumuishi 2026 yaliyofanyika katika kanisa la Waadventista Wasabato Maganzo, yakihusisha waumini kutoka katika maeneo mbalimbali ya Field ya Mkoa wa Shinyanga na Geita.


Katika hafla hiyo, Mhe. Tandiko amewataka waumini na wananchi kwa ujumla kuendelea kuthamini amani iliyopo nchini na kuhakikisha upendo na mshikamano vinaendelea kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, akisisitiza kuwa hali hiyo ni muhimu kwa waumini kuendelea kutekeleza misingi ya ibada kwa uhuru na utulivu.


Aidha, amesema kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuhamasisha amani, upendo na mshikamano katika jamii, huku akiwapongeza waumini wa Sabatho (S.D.A) kwa kuendelea kuliombea taifa pamoja na kuwaombea viongozi wote ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa hekima, uadilifu na mafanikio.


Kwa upande wake, Mwakilishi wa Field ya Kanda hiyo, Mchungaji Paul Kwilasa, ameongoza maombi maalum yaliyolenga kuliombea taifa, viongozi na wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuiombea Tanzania ili iendelee kuwa na amani, utulivu na mshikamano.


Katika hafla hiyo, Mhe. Tandiko pia amekabidhiwa vitabu mbalimbali pamoja na kushiriki shughuli nyingine za kufunga Makambi Jumuishi 2026 yaliyodumu kwa juma moja yakilenga kuimarisha imani, umoja na mshikamano miongoni mwa waumini.


Makambi hayo yamekuwa sehemu muhimu ya kujenga umoja na kuimarisha misingi ya kiroho, huku ujumbe wa amani na mshikamano ukibeba nafasi kubwa katika kufunga rasmi shughuli hizo.







0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم