NAIBU KAMISHINA WA UTUNZAJI NYARAKA, ULINZI, AMANI NA USALAMA VYUONI TAHLISO AFANYA ZIARA MAALUM OFISI YA KAMANDA WA JESHI LA MAGEREZA MKOA WA IRINGA (RPO)

 Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya uongozi wa wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama nchini, Ndugu Machunda Mwanishi Mishack , Naibu Kamishina wa Utunzaji Nyaraka, Ulinzi, Amani na Usalama Vyuoni wa TAHLISO, ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Iringa (RPO).


Ziara hiyo imefanyika kwa lengo la kujitambulisha rasmi, kujenga na kuimarisha mahusiano ya kiutendaji kati ya TAHLISO na Jeshi la Magereza, pamoja na kupata ushauri, maelekezo na malezi muhimu katika masuala ya ulinzi, amani, usalama, nidhamu na uzalendo.

Katika mazungumzo hayo, umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za elimu, viongozi wa wanafunzi na vyombo vya ulinzi na usalama ulipewa kipaumbele, hususan katika kuhakikisha taasisi za elimu zinabaki kuwa maeneo yenye amani, utulivu, mshikamano na mazingira salama ya kujifunzia.

Ziara hii pia ni sehemu ya utekelezaji wa maono na kipaumbele cha uongozi wa Rais wa TAHILISO, Mhe. Geofrey Kiliba, cha kuendelea kuhakikisha wanafunzi katika vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini Tanzania wanapata mazingira salama na rafiki yatakayowawezesha kutimiza malengo yao ya kielimu, huku wakijengewa misingi imara ya nidhamu, uzalendo, uwajibikaji na kuheshimu sheria za nchi.

TAHLISO inaamini kuwa usalama na amani katika mazingira ya vyuo ni msingi muhimu wa maendeleo ya taaluma na ustawi wa wanafunzi. Kupitia ushirikiano na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama, TAHILISO itaendelea kujenga daraja la mawasiliano, ushirikiano na malezi bora kwa manufaa ya wanafunzi na taifa kwa ujumla.

Ushirikiano imara kati ya wanafunzi na vyombo vya ulinzi ni hatua muhimu katika kujenga kizazi chenye nidhamu, uzalendo na uwajibikaji kwa Taifa.



0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم