NANGI AWAASA VIJANA KUTUMIA MICHEZO KUJENGA VIPAJI NA FURSA ZA KIUCHUMI

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Jenipha Nangi akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Nkwembele Cup Pemba Fc ya kijiji cha Mangu Kata ya Shagihilu Agosti 23, 2026 kabumbu lililosakatwa katiaka viwanja vya Shule ya msingi Mwanulu iliyoichapa Madrid Fc bao 1-0

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Jenipha Nangi akizungumza alipokuwa mgeni rasmi wa kufunga ligi ya Nkwembele Cup ya Kijiji cha Mwanulu Agosti 23,3036 katika viwanja vya shule ya Msingi Mwanulu


Na Sumai Salum-Kishapu


Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Jenipha Nangi, amewataka vijana kutumia michezo kama fursa ya kuibua vipaji, kujenga nidhamu, kuimarisha umoja na kujitengenezea fursa za kiuchumi.


Jenipha ameyasema hayo wakati akifungua rasmi mashindano ya Nkwembele Cup 2026 kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mwanulu yaliyoshirikisha timu 32 kutoka Kata mbalimbali za Wilaya hiyo, amesema michezo si burudani pekee, bali ni sehemu muhimu ya kuwaandaa vijana katika maisha, huku akiwataka kutumia vipaji vyao kwa manufaa yao binafsi na maendeleo ya jamii.


“Michezo si burudani tu, ni njia ya kujenga umoja, nidhamu na kuandaa viongozi wa kesho. Nikupongeze Mzee Robert Matius kwa uandaaji wa ligi hii kwani umeendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuinua sekta ya michezo na kuwafungulia vijana fursa za maendeleo na ajira kupitia vipaji vyao, pia
 jukwaa linawawezesha vijana kushiriki katika shughuli zenye tija".

Wachezaji wa timu ya Pemba Fc ya Kijiji cha Mangu Kata ya Shagihilu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi ya kufunga mashindano hayo Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo Jenipha Nangi Agosti 23,2026 katika viwanja vya michezo shule ya msingi Mwanulu

Pemba FC ya Kijiji cha Mangu, Kata ya Shagihilu, imeibuka bingwa baada ya kuifunga Madrid FC ya Mwanulu Kata ya Mwataga bao 1-0 bao pekee la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Nado, mwenye jezi namba 7, katika dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza cha mchezo.


Kwa ushindi huo, Pemba FC imejinyakulia Kombe la Nkwembele Cup, pamoja na Shilingi milioni moja, huku Madrid FC ikiwa mshidni wa pili na kupewa Shilingi laki tano.


Mashindano hayo ya Nkwembele Cup yamehusisha jumla ya timu 32 kutoka kata mbalimbali za Wilaya ya Kishapu, yakilenga kuibua vipaji vya vijana na kuimarisha mshikamano kupitia michezo.
Wachezaji wa timu ya Madrid Fc ya Kijiji cha Mwanulu Kata ya Mwataga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi ya kufunga mashindano hayo Mwenyekiti wa UVCCM wilayani humo Jenipha Nangi Agosti 23, 2026 katika viwanja vya shule ya msingi Mwanulu
Kiungo namba saba Ramadhan Ally "Nado" wa timu ya Pemba  Fc ya Mangu aliyewachapa Madrid Fc bao 1 dakika ya 3 ya kipindi cha kwanza 
Mwandaaji wa ligi ya Nkwembele Cup Robert Matius



























































































































0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post