BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAJADILI UWAJIBIKAJI WA MENEJIMENTI MWAKA WA FEDHA 2025/2026, UKUSANYAJI MAPATO WAPEWA "HEKO"

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limejadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Menejimenti ya Halmashauri katika mwaka wa fedha 2025/2026 huku wakipongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu  Mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza.

Aidha kikao hicho kilichofanyika Septemba 10,2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo,wakuu wa vitengo na idara waliwasilisha taarifa za shughuli za utendaji wa Menejimenti ambapo Madiwani walipata nafasi ya kujadili kwa kina na kutoa maelekezo kwa ajili ya kuimarisha ufanisi wa Halmashauri kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. Josephat Limbe, amewashukuru madiwani kwa kujadili kwa kina taarifa zilizowasilishwa na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa pamoja.


“Yapo mafanikio ambayo ninakiri kama Mwenyekiti, kwa namna ambavyo tumeshirikiana kwa pamoja na Menejimenti yametupa matokea tunayoyaona hivi sasa kwenye Halmashauri yetu” amesema Limbe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, amewashukuru madiwani akisema majadiliano hayo yaliyotokana na taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya idara na vitengo yamewapa mwelekeo mpya kama Menejimenti wa kujitathmini na kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa, ili kuimarisha ustawi wa Halmashauri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza

Naye Diwani wa Kata ya Sekebugoro Mhe. Fredinand Mpogomi, ametoa pongezi kwa Halmashauri kutokana na taarifa iliyowasilishwa na Kitengo cha Fedha na Uhasibu, ambayo ilibainisha kuongezeka kwa kiwango cha makusanyo ya mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.


“Halmashauri yetu imepiga hatua katika makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo tulifikia asilimia 93 tunapaswa tujipongeze kwa hili, na tujipange sasa kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ili tufikie asilimia 100,” amesema Mpogomi.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana akizungumza.
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akifuatilia Baraza Hilo
















0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم