RC MTANDA AKABIDHIWA RASMI OFISI


MKUU wa Mkoa wa Simiyu Said Mtanda (kushoto) akipokea baadhi ya nyaraka na vitabu kama sehemu ya makabidhiano na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha (kulia).

Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mohamed Mtanda amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa huo Anamringi Macha, ambaye amestaafu utumishi wa Umma.

Hafla ya makabidhiano ya Ofisi imefanyika leo Tarehe 4 Septemba katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu iliyoko Nyaumata Wilayani Bariadi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ofisi, Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda amempongeza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo kwa kustaafu utumishi wa umma.

Ametoa wito kwa watumishi wa umma Mkoani Simiyu kumpa ushirikiano ili kuweza kutekeleza jukumu la kuwahudumia Wananchi ipasavyo.


0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم