
Shule ya Sekondari Maganzo wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, imefanya Mahafali ya Kidato cha Nne leo Oktoba 2, 2026, huku Mgeni Rasmi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kishapu, Jenipha Nangi, aliyemwakilisha Diwani wa Kata ya Maganzo, Mhe. Hamza Tandiko.
Katika mahafali hayo, Nangi amekabidhi jumla ya kompyuta nne (4) kwa Shule ya Sekondari Maganzo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono maendeleo ya elimu na matumizi ya teknolojia katika kujifunza.
Akizungumza katika hafla hiyo, Nangi amewapongeza wanafunzi wanaohitimu kwa kufikia hatua hiyo na kuwataka kuendelea kuwa na nidhamu, bidii na kutumia elimu waliyoipata kwa manufaa yao, familia na jamii kwa ujumla.









إرسال تعليق