BARRICK NORTH MARA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KATIKA MADINI KWA KUTOA MSAADA GEREZA LA TARIME NA KWENYE JAMII


Mkuu wa Wilaya, Meja Edward Gowele (aliyevaa shati la bluu), viongozi wa Gereza la Tarime na wafanyakazi wanawake kutoka Barrick North Mara wakiwa katika hafla ya kukabidhi misaada gerezani hapo.
Wafanyakazi wa Barrick North Mara wakikabidhi misaada mbalimbali kwa jamii.
Wafanyakazi wa Barrick North Mara wakikabidhi misaada mbalimbali kwa jamii.
Wafanyakazi wa Barrick North Mara wakikabidhi misaada mbalimbali kwa jamii.
Wafanyakazi wa Barrick North Mara wakikabidhi misaada mbalimbali kwa jamii.

**
Katika kuadhimisha siku ya wanawake kwenye sekta ya madini duniani, wafanyakazi wanawake kutoka Mgodi wa Barrick North Mara na wakandarasi wametembelea Gereza la wanawake la Tarime mkoani Mara na kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali.

Mbali na kupeleka msaada kwenye gereza la Tarime pia wamepeleka misaada mingine ya kibinadamu kwa familia 60 katika jamii ya vijiji vilivvo jirani na mgodi huo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele ambaye amewashukuru wafanyakazi hao wa Barrick North Mara kwa moyo wa upendo, huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo wa kusaidia makundi mbalimbali yenye mahitaji katika jamii.

Misaada iliyotolewa kwenye gereza la Tarime kwa ajili ya kuwasaidia mahabusu na wafungwa wanawake ni pamoja na magodoro 25, blanketi 25, taulo za kuogea 25, vitenge pea 50, sabuni za kuogea katoni 25, ndala pea 25, dawa za meno pakti 48, sabuni za kufulia mifuko mitano na taulo za kike 372.

Orodha ya misaada hiyo pia imehusisha unga wa mahindi kilo 300, maharage kilo 100, mchele kilo 50, chumvi pakti 63 na mabati 50.

Aidha, wafanyakazi hao wanawake wamempatia mfungwa mwenye mtoto wa umri wa miezi 11 gerezani hapo misaada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nguo za mtoto pea 13, viatu vya mtoto pea mbili, sweta pea tatu, sabuni 12 za kuogea za mtoto, pampers boksi 10 na mafuta ya kujipaka.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake kwenye sekta ya madini duniani,kampuni ya Barrick inatumia siku hii kama jukwaa la kutathimini na kuendeleza juhudi za wanawake kazini,kusaidia jamii zinazozunguka migodi na kuchochea wanawake kuingia katika sekta ya madini ambayo awali kwa kiasi kikubwa ilitawaliwa na wanaume.

Juhudi za uwezeshaji wanawake zinaendana sambamba na sera ya serikali ya kuogeza ushirikishwaji wa watanzania (Local content) na kuimarisha uwakilishi wa wanawake katika mnyororo wa sekta ya madini.

Mgodi wa Barrick North Mara na wakandarasi wake wametoa ajira nyingi kwa wanawake, wengi wao wakiwa ni kutoka vijiji vilivyo jirani na mgodi huo.








0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم