SKAUTI WASISITIZWA KUZINGATIA MAADILI, MIIKO NA MIONGOZO


Na COSTANTINE MATHIAS-MASWA


‎KAMISHNA wa Skauti Mkoa wa Simiyu, Mkaguzi wa Polisi, Francis Seth Msuku, amewataka Vijana wa Chama Cha Skauti kuhakikisha wanaishi kwa kuzingatia Maadili, Miiko ma miongozo ya Skauti, pamoja na kuonyesha Maadili mema kwa viongozi, wazazi na Walezi.


‎Kamishna huyo ameyasema hayo jana kwenye Uzinduzi wa Kambi ya Skauti Mkoa wa Simiyu inayofanyika katika Shule ya msingi St. Aloyce Gonzaga iliyoko Shanwa wilayani Maswa ambapo alisema kupitia mafunzo hayo ya kielimu vijana watajengewa uwezo wa kumudu stadi za maisha hasa ukakamavu na kujitegemea.

"Katika Skauti tunafundisha uzalendo, kuipenda nchi yetu, tunaishi kama kaka na dada, kwenueafunzo yetu tunatoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia... na baada ya mafunzo haya tutawatunuku nishani za impesa kwa vijana 12 watakaofanya vizuri, skauti inawajenga vijana kuwa raia wema na wazalendo na tunatakiwa kuwa na umahiri katika umaridadi" amesema Kamishna huyo na kuongeza.

‎"Tutafundisha maadili, uraia mwema, mmomonyoko, tunafundisha watoto kuwa jasiri na wanapata mwamko wa kujisimamia mafunzo na kambi hii ni muhimu sana...Taasisi mbalimbali ikiwemo Polisi, Zimamoto, Takukuru, Maafisa Lishe watafundisha kitojihusisha na ukatili, madawa ya kulevya, Uzalendo na kuwajenga waweze kujisimamia wenyewe na kupitia makambi haya wanapata stadi mbalimbali za maisha."

‎Msuku amesema kuwa kupitia Kambi hizo, wanajifunza na kufanya maandalizi kwa ajili ya kushiriki kwenye mafunzo ya Kitaifa Mkoani Dodoma, huku akiwataka wadau kufanikisha upatikanaji wa jola sita kwa ajili ha sare za vijana hao pamoja na chakula ili kuendeshea Kambi hiyo.

‎‎Awali Mkufunzi wa Skauti (ALT) Mwalimu James Rweyemamu amesema kupitia Mafunzo hayo wamelenga kupata vijana Bora watakaowakilisha kambi ya kitaifa ambapo wamelenga kuwashindanisha ili kupata vijana mahili ambao watasajiliwa kwenye mfumo.

‎"Moja ya sharti la vijana wetu lazima wawe na sare, tunazingatia misingi ya nidhamu...Skauti hatuna Mme na mke, tuna matron anayesimamia usalama wa Wasichana, tunafundisha uzalendo, kujituma, Uwajibikaji na kulinda Tunu za Taifa" Ameeleza Mwalimu Rweyemamu.

Skauti kutoka Meatu 
Pawa Sayi amesema kupitia makambi hayo watajifunza uzalendo wa maisha pamoja na kufundishwa mbinu mbalimbali za kutatua changamoto katika maisha yao ya kila siku.

‎Naye Lusia Seni, Skauti kutoka wilaya ya Maswa, amesema kuwa kambi hiyo itawasaidia vijana kuwa wazoefu na kuwa wabunifu, huku akiwataka wazazi kutozuia watoto kupelekwa Skauti.

Mgeni Rasmi katika Ufunguzi, Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Simiyu, David Wambura amewataka Vijana hao kuwa na Nidhamu, kujenga Maadili, Ushupavu, Uzalendo kwa lengo la kulitumikia taifa.

‎"Tunajenga vijana kuwa na nidhamu, Taifa linajengwa na Watu shupavu, wazalendo, si wengine ni Skauti, wanajengwa...wajibu wenu ni kupokea Kwa nidhamu mnayoelekezwa, tupendane, Upendo utawale na msikengeuke kuwa na wizi, myaishi mtakayofundishwa ili yatusaidie katika makuzi na shughuli zetu, ikatusaidie katika maandalizi ya kupata ushindi Dodoma." amesema na kuongeza.

‎"Mkaheshimu wakubwa, wazazi na walezi , kupitia Kambi hii itawajengea uzalendo, mtapata nasaha za Maadili mema, kupitia Skauti tutapata vijana wa kuitumikia nchi yao wakiwa katika hali ya ukakamvu na wasiendane na matendo maovu, wakufunzo mkawatengenezee Mazingira wasijingize katika magenge mabaya, wawe taa na mwanga kwa vijana wenzao...tuwe chanzo cha kuwasaidia walioko mtaani, tuwe vijana tunaomuunga mkono Rais Dk. Samia ili tuendeleze tunu ya amani"


‎Katika kambi hiyo hiyo ya Kielimu ya skauti jumla vijana 280 wakiwemo Wasichana 88 na wavulana 112 wamejiunga kushiriki mafunzo hayo.








0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم