Meneja Miradi Shirika la TCRS mkoani Shinyanga Dkt. Oscar Rutenge
Na Sumai Salum- Kishapu
Shirika la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) kwa ufadhili wa fedha kutoka Norwegian Church Aid (NCA) limeendesha mafunzo ya siku moja kuhusu Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia (Gender Responsive Budgeting - GRB) kwa viongozi na wadau wa maendeleo kutoka Kata za Shagihilu na Ndoleleji, wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuimarisha usawa wa kijinsia na maendeleo jumuishi katika jamii.
Mafunzo hayo yamefanyika Juni 23, 2026 katika Shule ya Msingi Ndoleleji yakilenga kuimarisha uelewa wa viongozi na wadau wa maendeleo kuhusu umuhimu wa kuandaa na kutekeleza bajeti zinazozingatia mahitaji ya makundi yote katika jamii kwa usawa.
Washiriki ni pamoja na Waheshimiwa Diwani Kata ya Shaghihilu, Diwani wa Kata ya Ndoleleji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Afisa Watendaji wa Kata za Shaghihilu na Ndoleleji, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata za Shaghihilu na Ndoleleji. Aidha washiriki wengine ni Wenyeviti wa vijiji, Afisa Watendaji wa vijiji, Wawakilishi wa Madhehebu ya Dini, Wawakilisha wa watu wenye ulemavu na wakalishi wa Wanawake . Wote kutoka vijiji vya Mwalata, Ndoleleji, Shaghihilu na Mangu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, mwezeshaji wa programu hiyo, Dkt. Oscar Rutenge, amesema kuwa uandaaji wa mipango shirikishi yenye mtazamo wa kijinsia ni nyenzo muhimu katika kuleta maendeleo endelevu na kuboresha mfumo wa bajeti katika ngazi za Kata na Vijiji.
Ameeleza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kuweka mikakati inayolenga kuimarisha usawa wa kijinsia na kuhakikisha wananchi wanapata haki na fursa sawa katika maendeleo.

Mwenzeshaji wa mada iliyohusu Bajeti katika mtazamo wa kijinsia ( Gender Responsive Budgeting -GRB) Stephen Rusimbi akiendelea kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusiana na umuhimu wa kuandaa na kutekeleza bajeti zinazozingatia mahitaji ya makundi yote katika jamii kwa usawa Juni 23, 2026 shule ya msingi Ndoleleji wilayani Kishapu mkoani Shinyanga mafunzo yaliyoratibiwa na Shirika la TCRS mkoani humo
Mwezeshaji wa mafunzo Stephen Rusimbi amesisitiza kuwa lengo la Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia si kuandaa bajeti pekee, bali kuhakikisha utekelezaji wake pamoja na tathmini vinafanyika kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia katika jamii.
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo ambao ni viongozi na wajumbe wa kamati mbalimbali za maendeleo wamekumbushwa wajibu wao katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya maendeleo kwa kushirikiana na Serikali.
Rusimbi ametaja ukosefu wa taarifa na takwimu sahihi kuwa miongoni mwa changamoto zinazoathiri upangaji wa bajeti zenye tija. Amesisitiza umuhimu wa serikali za vijiji kuwa na takwimu sahihi zilizogawanywa kwa makundi mbalimbali ya kijamii ili kubaini changamoto zinazowakabili wananchi na kupanga suluhisho stahiki kwa ufanisi zaidi.
Amesema matumizi ya takwimu sahihi yatawezesha upangaji wa bajeti unaojibu mahitaji halisi ya wananchi na hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata wakisema itawasaidia kuboresha ushiriki wao katika mipango na bajeti zenye usawa na za maendeleo katika maeneo yao.
“Kwa muda mrefu tulikuwa tunaangalia bajeti kama jambo la wataalamu pekee, lakini leo tumeelewa kuwa kila mwananchi ana nafasi ya kutoa mawazo yake. Tumejifunza namna ya kuhakikisha wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu wanazingatiwa katika mipango ya maendeleo,” amesema Nickson Limbe kutoka Shagihilu
Edward Emmanuel Kutokea Kata ya Ndoleleji wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja kuhusu iliyoratibiwa na Shirika la TCRS kuhusu Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia yaliyofanyika Juni 23,2026 shule ya msingi Ndoleleji yakihusisha Kata ya Shagihilu na Ndoleleji wilayani humo
Naye Edward Emmanuel, ambaye ni mtu mwenye ulemavu kutoka Kata ya Ndoleleji, amesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwake na kwa watu wenye mahitaji maalumu kwani yamewapa uelewa kuhusu nafasi yao katika mchakato wa kupanga na kusimamia maendeleo,.Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia inasaidia kuhakikisha hakuna kundi linaloachwa nyuma katika maendeleo, hususan watu wenye ulemavu, wanawake, wazee na vijana.
Naye mshiriki mwingine kutoka Kijiji Cha Mwatuju Kata ya Shagihilu, Rehema Tambaru Mboje, amesema elimu hiyo itasaidia viongozi kufanya maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wote na kuondoa changamoto zinazotokana na kutoweka kwa usawa katika ugawaji wa rasilimali huku yakiwaongezea ujasiri wanawake kushiriki kikamilifu katika mijadala ya maendeleo na kutoa maoni yao bila woga.
Amebainisha kuwa elimu hiyo inapaswa kuwafikia watendaji wa vijiji, wenyeviti wa vijiji na madiwani wa kata, kwa kuwa wao ni miongoni mwa wahusika wakuu katika kuidhinisha na kusimamia mipango ya maendeleo ya Halmashauri.
“Kuna wajibu mkubwa kwa wataalamu wa Halmashauri kuhakikisha mipango na rasilimali zinaakisi masuala ya kijinsia kwa kukusanya, kuchambua na kutumia takwimu zilizochambuliwa kijinsia. Pia wanapaswa kurahisisha mifumo ya maombi ya mikopo bila vikwazo na kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa afua za kijamii zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa,” amesema Rusimbi.
Nickson Limbe Mola kutokea Kata ya Shagihilu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoratibiwa na Shirika la TCRS kuhusu Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia yaliyofanyika Juni 23,2026 shule ya msingi Ndoleleji yakihusisha Kata ya Shagihilu na Ndoleleji wilayani humo
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo ambao ni viongozi na wajumbe wa kamati mbalimbali za maendeleo wamekumbushwa wajibu wao katika kusimamia na kutekeleza majukumu ya maendeleo kwa kushirikiana na Serikali.
Rusimbi ametaja ukosefu wa taarifa na takwimu sahihi kuwa miongoni mwa changamoto zinazoathiri upangaji wa bajeti zenye tija. Amesisitiza umuhimu wa serikali za vijiji kuwa na takwimu sahihi zilizogawanywa kwa makundi mbalimbali ya kijamii ili kubaini changamoto zinazowakabili wananchi na kupanga suluhisho stahiki kwa ufanisi zaidi.
Amesema matumizi ya takwimu sahihi yatawezesha upangaji wa bajeti unaojibu mahitaji halisi ya wananchi na hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata wakisema itawasaidia kuboresha ushiriki wao katika mipango na bajeti zenye usawa na za maendeleo katika maeneo yao.
“Kwa muda mrefu tulikuwa tunaangalia bajeti kama jambo la wataalamu pekee, lakini leo tumeelewa kuwa kila mwananchi ana nafasi ya kutoa mawazo yake. Tumejifunza namna ya kuhakikisha wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu wanazingatiwa katika mipango ya maendeleo,” amesema Nickson Limbe kutoka Shagihilu
Naye Edward Emmanuel, ambaye ni mtu mwenye ulemavu kutoka Kata ya Ndoleleji, amesema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwake na kwa watu wenye mahitaji maalumu kwani yamewapa uelewa kuhusu nafasi yao katika mchakato wa kupanga na kusimamia maendeleo,.Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia inasaidia kuhakikisha hakuna kundi linaloachwa nyuma katika maendeleo, hususan watu wenye ulemavu, wanawake, wazee na vijana.
Naye mshiriki mwingine kutoka Kijiji Cha Mangu Kata ya Shagihilu, Rehema Tambaru Mboje, amesema elimu hiyo itasaidia viongozi kufanya maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wote na kuondoa changamoto zinazotokana na kutoweka kwa usawa katika ugawaji wa rasilimali huku yakiwaongezea ujasiri wanawake kushiriki kikamilifu katika mijadala ya maendeleo na kutoa maoni yao bila woga.
Washiriki hao kwa pamoja wameishukuru TCRS kwa kuendelea kuwajengea uwezo viongozi na wananchi katika masuala ya maendeleo, wakisema elimu hiyo itasaidia kuongeza uwajibikaji, ushiriki wa wananchi na usawa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya ya Kishapu.
Rehema Tambaru Mboje (aliyekaa kushoto) kutokea Kijiji Cha Mwatuju Kata ya Shagihilu Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoratibiwa na Shirika la TCRS kuhusu Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia yaliyofanyika Juni 23,2026 shule ya msingi Ndoleleji yakihusisha Kata ya Shagihilu na Ndoleleji wilayani humo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na Diwani wa Kata ya Ndoleleji Mhe. Josephat Limbe akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoratibiwa na Shirika la TCRS kuhusu Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia yaliyofanyika Juni 23,2026 shule ya msingi Ndoleleji yakihusisha Kata ya Shagihilu na Ndoleleji wilayani humo
Diwani wa Kata ya Shagihilu Mhe. Deogratius Seni Nicasius akizungumza wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoratibiwa na Shirika la TCRS kuhusu Bajeti katika Mtazamo wa Kijinsia yaliyofanyika Juni 23,2026 shule ya msingi Ndoleleji yakihusisha Kata ya Shagihilu na Ndoleleji wilayani humo
إرسال تعليق