PICHA: SHY TOWN VETERAN MSHINDI BONANZA LA MICHEZO SABASABA KISHAPU

Na Sumai Salum-Kishapu

Timu ya Shy Town Veteran imeandika historia kwa kutwaa ubingwa wa Bonanza la Michezo la Sabasaba Kishapu 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simiyu Veteran. Bao la ushindi lilifungwa dakika ya 25 ya kipindi cha pili, na kuifanya Shy Town Veteran kutwaa taji hilo katika bonanza lililoratibiwa na Kishapu Veteran, likizikutanisha timu mbalimbali za veteran. Mashindano hayo yalifanyika tarehe 11–12 Julai, 2026 katika viwanja vya Shule ya Msingi Buduhe.

Mashindano hayo yamefungwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, ambaye amewapongeza washiriki wote kwa kuonesha ushindani wa hali ya juu, mshikamano na kudumisha afya kupitia michezo huku akiwakumbusha kuhusu fursa za kiuchumi na kijamii zilizoko wilayani humo.

Kauli mbiu ya bonanza hilo ni "Amani na utulivu Kishapu ni Tunu ya Taifa"
Mkuu wa Wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akikabidhi kombe kwa msindi wa kwanza wa mpira wa miguu Shy Town Veteran kwenye bonanza la michezo la sabasaba lililoanza Julai 11 na kumalizika Julai 12, 2026 lililoratibiwa na Kishapu Veteran na kufanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Buduhe wilayani humo 
Mkuu wa Wilaya ya kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye bonanza la michezo la sabasaba lililoanza Julai 11 na kumalizika Julai 12, 2026 lililoratibiwa na Kishapu Veteran na kufanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Buduhe wilayani humo huku likizikutanisha timu tano za maveterani kutokea mikoa ya Mwanza, Shinyanga,Simiyu na Tabora
Kiungo wa timu ya Shy Town Veteran Wahabi Mchome winga namba 11 aliyewapa ushindi timu yake wa bao 1 dhidi ya 0 (Simiyu) dakika ya 25 kipindi cha pili cha mchezo huo
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akifuatilia mchezoPicha ya pamoja ya Mgeni rasmi wa mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi na wachezaji wa timu ya Shy Town Veteran
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi wa mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi na waamuzi wa mechi

Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi wa mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi na wachezaji wa timu ya Simiyu Veteran





Tazama picha za wananchi mbalimbali wakifuatilia mchezo huo wa Shy Town Veteran dhidi ya Simiyu Veteran 











 




























































Picha mbalimbali Mkuu wa Wilaya Mhe. Peter Masindi akikagua timu hizo


































Picha mbalimbai a upokeaji Kombe, vyeti na medali baada ya mchezo














































Picha baada ya kupokea Komboe, cheti na medali









































0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم