Na Sumai Salum-Kishapu

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 204.7 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100, utakaotekelezwa katika eneo la Ngunga, Wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga.
Mkataba huo umesainiwa leo, Julai 27, 2026 katika Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga wilayani humo, kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na mkandarasi anayetekeleza mradi huo, kampuni za Sagemcom Energy & Telecom SAS na STEG International Services utakaotekelezwa kwa muda wa miezi kumi na saba (17).
Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb), akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 204.7 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu mkoaani Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100 katika Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga Julai 27, 2026
Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri Ndejembi amesema mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha mseto wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme (energy mix), kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, wa gharama nafuu na unaotokana na vyanzo vya nishati jadidifu.
Ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili zenye uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawati 150. Awamu ya kwanza yenye uwezo wa Megawati 50 iligharimu Shilingi bilioni 118.3 na kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za utekelezaji.
Kwa mujibu wa Waziri Ndejembi, awamu ya pili yenye uwezo wa Megawati 100, ambayo utekelezaji wake umeanza rasmi kupitia utiaji saini wa mkataba huo, itagharimu Shilingi bilioni 204.7, na kufanya gharama za jumla za mradi kufikia Shilingi bilioni 323.
Amesema mradi huo utachangia kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo vya nishati jadidifu, kuimarisha uthabiti wa mfumo wa umeme nchini na kusaidia Serikali kufikia malengo ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye.
Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya nishati kwa lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na wa gharama nafuu. Akieleza kuwa lengo la Serikali si kujenga miradi pekee, bali kuhakikisha usalama wa nishati kwa vizazi vya sasa na vijavyo, kuongeza ushindani wa uchumi, kuvutia uwekezaji, kuimarisha shughuli za uzalishaji na kufungua fursa zaidi za ajira kwa Watanzania.
"Nisisitize kwenu Tanesco hakikisheni mnawasimamia wakandarasi kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa wakati na kwa ubora unaokidhi matarajio ya Serikali na wananchi huku pia mkiwapa kipaumbele vijana wazao ambao walihusika kwenye mradi uliopita kuhakikisha wanapata ajira ili wanufaike pia na mradi huo." Ameongeza
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Lazaro Twange akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 204.7 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu mkoaani Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100 katika Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga Julai 27, 2026
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Bw. Lazaro Twange, amesema kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu Awamu ya Pili wenye uwezo wa kuzalisha megawati 100 ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mkakati wa TANESCO wa kuongeza uzalishaji wa umeme kupitia vyanzo vya nishati jadidifu.
"Mhe. Waziri mradi huu wenye thamani ya shilingi bilioni 204.7 utaongeza uimara wa Gridi ya Taifa, kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na sekta za uzalishaji, pamoja na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya maendeleo nipende kuahidi kuwa TANESCO tutasimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huu ili ukamilike kwa wakati, kwa ubora na kwa kuzingatia viwango vyote vya kitaalamu"ameongeza Bw. Twange.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 204.7 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu mkoaani Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100 katika Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga Julai 27, 2026
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, amesema utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu Awamu ya Pili unaonesha imani kubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwa nayo kwa Mkoa wa Shinyanga kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji na ushirikiano wa wananchi.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano kwa TANESCO, mkandarasi na wadau wote wa mradi ili kuhakikisha utekelezaji wake unakwenda kwa wakati, huku akiwahimiza wananchi kuendelea kulinda miundombinu ya umeme kwani ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya Taifa na ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.
Balozi mdogo wa Ufaransa Nchini Tanzania Jean Traband
akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini wa mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 204.7 kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu mkoaani Shinyanga wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100 katika Kijiji cha Ngunga Kata ya Talaga Julai 27, 2026
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba









إرسال تعليق