ZIARA YA KAMATI YA FEDHA, UTAWALA NA MIPANGO KISHAPU, YADHIHIRISHA UTENDAJI KAZI WA SERIKALI KWA WANANCHI

     
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Lucy Mayenga akiwa na Kamati ya Fedha Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakati wa ziara ya siku mbili ya kamati hiyo yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Julai 21-22, 2026
Mwenyekiti wa Halmasahuri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango Mhe. Josephat Limbe akizungumza wakati wa ziara hiyo ya siku mbili kuanzia Julai 21-22, 2026

Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Josephat Limbe, kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Lucy Mayenga, imefanya ziara ya siku mbili Julai 21–22, 2026 ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na mtambo wa Excavator unaomilikiwa na Halmashauri.
Ziara hiyo imelenga kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa miradi, kujiridhisha na ubora wa kazi zinazotekelezwa, pamoja na kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanazingatia thamani halisi ya fedha (Value for Money).


Miradi iliyotembelewa ni pamoja na kikundi cha ufugaji wa mbuzi Mwamashele, ujenzi wa matundu sita ya choo, kichomea taka na mfumo wa maji katika Zahanati ya Ngofila, umaliziaji wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Ngunga, umaliziaji wa Zahanati ya Ikonokelo, ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na matundu ya choo katika Shule ya Msingi Bukingwamandege, kikundi cha vijana wa bodaboda Maganzo, pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya choo katika Shule ya Msingi Bulima.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu ya choo katika Shule ya Msingi Mwamasololo, umaliziaji wa vyumba viwili vya maabara katika Shule ya Sekondari Bunambiyu, pamoja na ujenzi wa matundu matano ya choo, kichomea taka na mfumo wa maji katika Zahanati ya Itongoitale.


Kamati imeeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika baadhi ya miradi huku ikitoa maelekezo kwa wataalamu na wakandarasi kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyowekwa ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ziara hiyo inaonesha dhamira ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na viongozi wake ya kuendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuhakikisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi wa wilaya hiyo.

 


Baadhi ya Wanafunzi wa Dalasa la Sita Shule ya Msingi Bukingwamandege wakifurahia uboreshewaji wa miundombinu ya Madalasa 

Wanafunzi wa Dalasa la tatu shule ya msingi Bukingwamandege wakifurahia miundombinu bora ya kujifunzia shuleni hapo

Picha za miradi mbalimbali liyotembelewa
























Jengo hili (picha ya chini) lilijengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Shule ya Msingi Bukingwamandege-Haukuwa miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kukaguliwa









































































































 

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم