.jpeg)
.jpeg)
Mkurugenzi wa mipango na uwekezaji wa TPDC Derick Moshi akizungumza

.jpeg)
Meneja wa kituo cha kusukuma mafuta ghafi namba tatu Dmitry Malyshev akizungumza

Na Mbuke Shilagi Kagera
Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi Namba Tatu (PS3) kinachojengwa katika Kijiji cha Kikagate, Kata ya Mubunda, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, kimefikia asilimia 88 ya ujenzi na kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Agosti au mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.
Kituo hicho ni sehemu ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) unaounganisha maeneo ya uzalishaji mafuta nchini Uganda na Tanzania.
Akizungumza wakati wa ziara ya wabia na wadau wa mradi kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa TPDC, Derick Moshi, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, amesema kufikia asilimia 88 ni hatua kubwa katika utekelezaji wa mradi huo.
Amesema TPDC, ambayo inamiliki asilimia 15 ya hisa katika EACOP, imeendelea kupata uzoefu kupitia mradi huo, hususan katika ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwenye uwekezaji na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati.
EACOP inamilikiwa na TotalEnergies kwa asilimia 62, UNOC asilimia 15, TPDC asilimia 15 na CNOOC Limited ya China asilimia 8.
Kwa upande wake, Meneja wa Kituo cha PS3, Dmitry Malyshev, amesema ujenzi ulianza Aprili 2024 na awali ulipangwa kukamilika Julai 2026, lakini changamoto za upatikanaji na ucheleweshaji wa malighafi zilisababisha kubadilika kwa ratiba.
Malyshev amesema kwa sasa kazi zilizobaki zinaendelea na kituo hicho kinatarajiwa kuwa tayari mwishoni mwa Agosti au mwanzoni mwa Septemba.
Aidha, matarajio ni kuona vituo vyote vya kusukuma mafuta vya EACOP vikikamilika ifikapo Desemba 2026, hatua itakayowezesha kukamilisha maandalizi ya kuanza uendeshaji wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

إرسال تعليق