WANANCHI MAGALATA WAIBUA KERO ZA BARABARA, SOKO NA KIVUKO KUELEKEA MVUA ZA EL NINO

-Maswali yajibiwa

-Mkuu wa Wilaya atoa maelekezo

Na Sumai Salum-Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026

WANANCHI wa Kijiji cha Magalata, Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wameiomba Serikali kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, kivuko pamoja na soko la kila siku, huku wakitaka hatua za haraka zichukuliwe kabla ya kuanza kwa mvua zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki kuelekea mwezi Oktoba.


Akizungumza katika mkutano wa hadharawa Mkuu wa Wilaya na Wananchi wa Kijiji hicho Septemba 30, 2026, Aziza Khamisi, mkazi wa Magalata, ameomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa soko la kila siku pamoja na kujenga kivuko kitakachotumiwa na wananchi kuelekea katika eneo la bwawa la samaki, akieleza kuwa huduma hizo zitasaidia shughuli za kiuchumi na kurahisisha maisha ya wananchi.


Mkazi mwingine Emmanuel Lyema, ameiomba Serikali kuwajengea barabara itakayounganisha Kata ya Mwamalasa na Wilaya ya Igunga ili kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na kuwawezesha wananchi kufika katika maeneo mbalimbali kwa urahisi.


Naye Robert Sango, mkazi wa eneo hilo, ameiomba Serikali isimamie kwa karibu mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara ya Gimagi-Mwamalasa, akisisitiza umuhimu wa kazi hiyo kukamilishwa kwa wakati kabla ya mvua za mwezi Oktoba ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua.
Katibu Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fatma Mohamed akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo na wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026


Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Magalata, Paul Makelebende, amesema wananchi wako tayari kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa miundombinu bora itakayochochea shughuli za kiuchumi katika kijiji hicho.


Diwani wa Kata ya Mwamalasa, Mhe. Bushi Mpina, amesema tayari Serikali ya Kata imeanza mikakati ya ujenzi wa soko la kila siku, huku akieleza kuwa hatua mbalimbali zimechukuliwa kuhakikisha eneo la soko linapatikana kwa kuzingatia taratibu na mahitaji ya wananchi.


"Kuhusu soko, Mkuu wa Wilaya rayari mazungumzo na maridhiano yamefanyika kuhusu eneo la ujenzi wa soko hilo, ikiwemo suala la mipaka na eneo la shule, hivyo hatua zinazofuata zinapaswa kuzingatia taratibu ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa usalama na uendelevu." Ameongeza
Diwani wa Kata ya Mwamalasa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Bushi Mpina, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa Wilaya hiyo wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026

Katika hatua nyingine, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Kishapu, Cecilia Lucas, amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika kampeni ya “Mjue Jirani Yako”, kwa kuwafahamu watu wanaoishi katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa mamlaka pale wanapobaini uwepo wa mtu asiyejulikana au mwenye taarifa zisizoeleweka.


Cecilia amesema kampeni hiyo inalenga kuimarisha usalama na ulinzi katika jamii kwa kujenga utamaduni wa wananchi kufahamiana, kushirikiana na kuwa na uelewa wa watu wanaoishi katika maeneo yao, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka husika kwa wakati.


Aidha, amewahimiza wananchi kuhakikisha wanapata Vitambulisho vya Taifa (NIDA), akieleza kuwa kitambulisho hicho ni muhimu katika utambulisho wa mtu na upatikanaji wa huduma mbalimbali. "kwa wale ambao bado hawajapata huduma ya NIDA wanapaswa kujiandikisha na pindi wanapofikisha idadi ya watu 50, taarifa hizo zifikishwe katika ofisi husika ili kwa kushirikiana na NIDA, watumishi waweze kuwafikia wananchi hao na kutoa huduma katika maeneo yao" amesema.


Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa kwa wakati kuhusu mahitaji yao ili Serikali iweze kuyafanyia kazi kwa kuzingatia vipaumbele na uwezo uliopo huku akisisitiza kuhusu upandaji miti kwa wingi na sio kukata miti.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, amejibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi na kutoa maelekezo kwa viongozi na watendaji kuhakikisha masuala yanayoweza kutatuliwa kwa hatua za haraka yanafanyiwa kazi kwa wakati.


Mhe. Masindi amesema barabara na madaraja ni miongoni mwa ngazi muhimu za maendeleo kwa kuwa zinawezesha wananchi kusafirisha mazao, kufikia huduma za kijamii na kuendesha shughuli zao za kiuchumi, akisisitiza kuwa katika utekelezaji wa miradi, Serikali itaendelea kuzingatia thamani ya fedha pamoja na ubora wa miradi kama vituo vya afya, madarasa, barabara na madaraja.


Mhe. Masindi pia amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua, ikiwemo kuhakikisha mashimo yote yaliyo wazi yanafukiwa ili kuzuia ajali, kuwalinda watoto na kuhakikisha usalama wa familia zao.
Afisa Uhamiaji wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Cecilia Lucas Matoboki akitoa elimu kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa Wilaya hiyo wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026


Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kuwa wamoja, kupendana na kumtegemea Mungu, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia zoezi la usafi wa mazingira linalofanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa jamii.


Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara za Mkuu wa Wilaya ya Kishapu katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, zinazolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi, pamoja na kuimarisha maandalizi ya jamii kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Niño.


Serikali imeendelea kuwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari mapema, kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kushirikiana na viongozi katika kutoa taarifa za maeneo hatarishi, huku wananchi wakihimizwa kutunza mazingira, kuimarisha miundombinu ya maeneo yao na kuhakikisha watoto pamoja na mali zao wanalindwa dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mvua.
Afisa Tawala wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Fadhili Mvanga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa Wilaya hiyo wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026
Mratibu wa maafa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Robert Mhina akitoa elimu jinsi ya kujilinda na majanga kwenye mkutano wa hadhara na Mkuu wa Wilaya hiyo wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026
Afisa Tarafa ya Kishapu mkoani Shinyanga Tano Malele akifatilia mkutano wa hadhara na Mkuu wa Wilaya hiyo wananchi wa Kijiji cha Magalata kilichoko Kata ya Mwamalasa wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili huku wakipewa elimu ya kukabiliana na el nino mkutano uliofanyika Septemba 30,2026
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Magalata, Paul Makelebende
Aziza Khamisi, mkazi wa Magalata
Emmanuel Lyema
Robert Sango




























































0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم