“ZERO MALARIA” YA BARRICK YAFIKIA KAYA ELFU 44 MSALALA

Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vyeti kwa washiriki wa zoezi la upuliziaji dawa majumbani kwenye mazalia ya mbu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Zero Malaria” unaolenga kuimarisha juhudi za kutokomeza ugonjwa wa malaria katika jamii zinazozunguka mgodi huo.

Mratibu wa Wadudu Wadhulifu ngazi ya Wilaya, Jullieth Petro, akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vyeti kwa washiriki wa zoezi la upuliziaji dawa majumbani kwenye mazalia ya mbu, yaliyoandaliwa katika kutekeleza mradi wa “Zero Malaria” unaofadhiliwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Mkurugenzi wa Gekahil, Bw. Gerald Elias, akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vyeti kwa washiriki wa zoezi la upuliziaji dawa majumbani kwenye mazalia ya mbu, yaliyoandaliwa katika utekelezaji wa mradi wa “Zero Malaria” unaofadhiliwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa lengo la kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria katika jamii.

Mratibu wa Wadudu Wadhulifu ngazi ya Wilaya, Jullieth Petro, akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa zoezi la upuliziaji dawa majumbani kwenye mazalia ya mbu, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria kupitia mradi wa “Zero Malaria” unaotekelezwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Gekahil, Bw. Gerald Elias (mwenye miwani), huku wa tatu kutoka kushoto akiwa ni Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo.

*****
Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga umeendelea na kampeni yake ya Kutokomeza Ugonjwa wa Malaria ijulikanayo kama “Zero Malaria” kwa kuwezesha kupuliza dawa kwenye mazalia ya mbu na majumbani kwenye kaya zipatazo 44,000 zilizopo kwenye kata za Bugarama na Bulyanhulu.

Akizungumza baada ya kuhitimisha zoezi la kupuliza dawa kwenye mazalia ya mbu na majumbani ambako limepongezwa na wananchi wengi, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala ambaye ni mratibu wa kupambana na wadudu wadhulifu ngazi ya wilaya , Julieth Petro amesema zoezi hilo limefanikiwa kufikia hizo kaya zilizopo kwenye kata mbili.

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu umekuwa ukiwezesha shughuli mbalimbali za kijamii , ikiwa ni pamoja na afua za afya kama vile upuliziaji wa dawa za mbu majumbani (Indoor Residual Spraying- IRS) ili kupambana na malari katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Akiongelea kampeni hiyo Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu , Zuwena Senkondo amesema lengo la zoezi hilo ni kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwa kuua na kutokomeza mazalia ya mbu kwenye kaya zilizopo karibu na mgodi na limekuwa likifanyika kila mwaka.

Senkondo amesema kuwa Barrick Bulyanhulu itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi sambamba na kuhakikisha wanakuwa na afya bora.

“Afya ni suala la muhimu katika jamii yoyote ile ndio maana Barrick Bulyanhulu tumekuja na kampeni ya kutokomeza ugonjwa hatari wa Malaria ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambao wamekuwa wahanga wakubwa wa ugonjwa huu na nina imani sote tukiungana pamoja tutafanikiwa kutokomeza ugonjwa huu”, amesema Senkondo.

Senkondo amefafanua kuwa, kupitia kampeni hii ya awamu ya kwanza mwaka huu , imeweza kuzifikia kaya elfu 44 katika makazi yao kwa kunyunyiziwa dawa za kuua mazalia ya mbu sambamba kugawiwa wananchi vyandarua.

Pamoja na mambo mengine amesisitiza kwamba aina ya dawa zinazotumika ni salama na zimeidhinishwa kwa matumizi ya nyumbani kama vile (Pyrethroids) na ufadhili huo unalenga kwenye vijiji na jamii inavyozunguka mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Zoezi hilo la Upuliziaji wa limeendeshwa na kampuni ya Gekahil Inter - Trade ltd huku vijana takribani 95 wakipata ajira za muda baada ya kushiriki zoezi hilo la zero malaria kampuni yenye kauli mbiu “Zero Malaria Inaanza na mimi , wewe na sisi sote”.

Mpango huu wa kupuliza dawa za kuua mbu, kugawa vyandarua vyenye dawa bure kwa wafanyakazi na jamii , utoaji wa elimu na kuhamasisha upimaji afya wa mara kwa mara umefanikisha kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria katika kata zinazozunguka mgodi wa Barrick Bulyanhulu.
Afisa Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Zuwena Senkondo, akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vyeti kwa washiriki wa zoezi la upuliziaji dawa majumbani kwenye mazalia ya mbu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Zero Malaria” unaolenga kuimarisha juhudi za kutokomeza ugonjwa wa malaria katika jamii zinazozunguka mgodi huo.

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم