ELIMU YA USONJI NA UMILIKI WA ARDHI: NJIA MPYA YA KUINUA WANAWAKE KIUCHUMI KISHAPU


Mkurugenzi wa Taswira ya Tumaini mkoani Shinyanga, Thomas Nyitati, akizungumza kwenye uzunduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani Kishapu mkoani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Peter Masindi akiwa ndiye mgeni rasmi

Na Sumai Salum - Kishapu

Elimu ya usonji na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake imeelezwa kuwa nguzo muhimu ya kuwawezesha wanawake kujitegemea, kutumia fursa zilizopo na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya familia na jamii.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Taswira ya Tumaini, Thomas Nyitati, wakati akitoa elimu ya usonji katika uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kishapu Julai 16, 2026. Nyitati amewataka wanawake kutumia maarifa wanayopata kubuni na kuendeleza shughuli za kiuchumi zitakazoboresha maisha yao.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Julai 16, 2026 katika ukumbi wa Kishapu  akiwa ndiye mgeni rasmi

Akizindua rasmi jukwaa hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, aliwahimiza wanawake kumiliki ardhi kama msingi wa kujenga uchumi imara na kuongeza usalama wa mali zao. Pia aliwakumbusha kuwa pamoja na kujikwamua kiuchumi, waendelee kutimiza wajibu wao katika malezi ya familia na kuchangia maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akishikana mkono na Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kujikwamua kiuchumi wilayani humo Pendo Sabanja wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo Julai 16, 2026 ukumbi wa Kishapu Sekondari












Elimu ya Usonji Yatajwa Kufungua Milango ya Uchumi kwa Wanawake Kishapu




KISHAPU: Mkurugenzi wa Taswira ya Tumaini, Thomas Nyitati, amesema elimu ya usonji ni nyenzo muhimu katika kuwawezesha wanawake kujitambua, kutumia fursa zilizopo na kujenga uchumi imara wa familia na jamii. Ametoa kauli hiyo wakati akitoa elimu katika uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi uliofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kishapu.




Nyitati aliwahimiza wanawake kutumia maarifa wanayoyapata kubuni na kuendeleza shughuli za kiuchumi zenye tija ili kuongeza kipato na kuboresha ustawi wa familia zao.




Akizindua rasmi jukwaa hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, aliwataka wanawake kujenga utamaduni wa kumiliki ardhi na mali nyingine za uzalishaji ili kuongeza uhuru wa kiuchumi na kuchangia maendeleo endelevu ya Taifa. Aidha, aliwasisitiza kutosahau wajibu wao katika malezi ya familia, kujenga maadili mema na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم